
Serikali kupitia Wizara
ya Kilimo imesema inaendelea kushirikiana na mashirika ya kigeni ambayo yanawekeza
katika masuala ya kilimo ili kumsaidia mkulima kujikwamua kiuchumi kupitia
vyama vya ushirika.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Idara
ya Usalama wa Chakula kutoka Wizara hiyo Elimpaa
Kiranga wakati wa mahojiano na wahabari mara baada ya uzinduzi wa wa
program ya miaka mitano ambayo imeandaliwa na shirika la Weeffect kutoka nchini Sweeden ambalo limekuwa likifanya kazi
na vyama vya ushirika hapa nchini.
Amesema kuwa serikali
ya awamu ya tano inahakikisha hatua hiyo
inawanufaisha wakulima wa jinsia zote ambao wamejiunga katika vikundi kwa ajili
ya kufanya shuighuli za kilimo ili kusaidia kuboresha maisha yao na Taifa kwa
ujumla.
Awali akizungumzia
mradi huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Weeffect George Onyango amesenma program ya
miaka mitano inatarajiwa kutumia kasi cha shilingi za kitanzania bilioni 120 kwa
ajili ya kufanya kazi na vyama vya ushirika vipatavyo 11 nchini Tanzanaia,huku
akiomba serikali kuweka mbinu na sheria za kilimo zitakazowezesha mkulima kutoka katika umasikini.
INSERT.3.ANGELA
MOSHI.
Post a Comment