0



 Image result for ndugulile picha

 Na.Martin Joseph
Wananchi wameombwa kupima kupima afya zao ili kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa shindikizo la macho kwani ugonjwa huo umekuwa ukisababisha athari kubwa nakupelekea watu kupata upofu wasioutalajia.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsi,Wazee na Watoto Dkt.FAUSTINE NDUGULILE alipokuwa akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya wiki ya kuongeza uelewa kuhusu ugonjwa wa shindikizo la macho yenye kaulimbiu isemayo “okoa uoni wa macho yako’’iliyoanza hapo jana na inatalajiwa kuhitimishwa Machi 7 mwaka huu duniani kote.
Amesema kuwa ugonjwa huo ni moja kati ya magonjwa ya macho yanayoshambulia mshipa wa fahamu wa binadamu unaopeleka mawasiliano ya uoni kwenye ubongo ili kuweza kutafsiri kile unachokiona hivyo unaweza ukamsababishia mtu kupata upofu wa taratibu na hatimaye kushindwa kuhona kabisa.
Pia ameeleza kuwa ugonjwa huo unachangia kwa asilimia 15 ya watu wasiiona na unawaathiri Zaidi watu wenye umri kuanzia  miaka 40 na Zaidi kwani wengi wao wamekuwa hawana tabia ya kuchunguza Afya za  macho kama inavyo shauriwa na wataalamu hivyo basi ni muhimu wananchi wakapima afya za macho angalau mara moja hasa hasa kwa makundi yaliyo hatarini kupatwa na ugonjwa huo.
Aidha kwa upande mwingine NDUGULILE amseema maadhimisho hayo yatakuwa niyakutoa elimu na upimaji wa Afya ya macho kwenye klinki za macho kwaiyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kilnki na  vituo vyote vya afya vilivypo hapa nchini  kwa lengo la  kupimwa na kuchungunzwa kama watakua na dalili zinazo sababisha ugonjwa huo ili waweze kupatiwa matibu haraka ilikuepukana na ugonjwa huo ambao ni tishio hapa nchini na duniani kote.

Post a Comment

 
Top