Shirikisho la vyama vya mogonjwa yasiyo ya kuambukiza
Tanzania(TANCDA) limetakiwa kuongeza juhudi za
kutoa elimu kwa wananchi juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwani
kufanya hivyo kutawezesha familia nyingi kutopata magonjwa hayo na hata kwa
wale ambao wameathirika kuwa na elimu sahihi ya kuyadhibiti magonjwa hayo.
Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa magonjwa yasiyo
yakuambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt.SARA MAONGEZI alipokuwa akipokea tunzo
ya kimataifa ya hamasa kwa jamii juu ya
ufahamu wa magonjwa yasiyo yakuambukiza ambayo imetolewa na shirikisho la
kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza (Global NCDs Alliance) wakishirikiana
na Falme za kiarabu za mji wa Sharja.
Amesema kuwa magonjwa hayo yamechangia kuongezeka kwa idadi
kubwa ya vifo hapa nchini na hata kuwa ni moja ya sababu za tishio la uhai wa
binadamu duniani kwa sasa kwani asilimia 27 ya wananchi wanaofaliki huwa
wanakufa kwa magonjwa hayo hivyo ni
muhimu shirikisho hilo kutoa elimu hiyo ili kuliepusha taifa kutumia fedha
nyingi katika kutibu magonjwa hayo na hata kuepusha watu wengi kufa mapema.
Pia Dkt SARA ametoa wito kwa wananchi kuzingatia elimu
wanayopewa kupitia taasisi mbalimbali na vyombo vya habari juu ya magonjwa
yasiyo ya kuambukiza kwani itawasaidia kuwaepusha na magonjwa hayo kwani
yanaatahri kubwa katika maisha yao.
Aidha ametoa pongezi kwa shirikisho la vyama vya magonjwa
yasiyo ya kuambukiza (TANCDA) pamoja chama cha waandishi wanaopambana na magonjwa
yasiyo ya kuambukiza (TJNCDF) kwa juhudi wanazo zifanya kwa kutoa elimu kwa
wananchi kwani juhudi hizo ndizo zilizo changia kupatatika kwa tuzo hiyo hivyo
waendelee kutoa elimu zaidi ili kuongeza nguvu kazi na hata kuimarisha uchumi
wa Taifa na jamii kiujumla.
Post a Comment