
Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) imewataka wafanyabiashara
wote nchini kuhakikisha wananamba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN NAMBA) kwani
kufanya hivyo itaongeza idadi ya walipa kodi na hata kupata taarifa sahihi za
walipa kodi wanaostahili kukadiliwa na kutozwa kodi ili kuchangia kukua kwa
pato la taifa.
Hayo yamesemwa na kamishina wa kodi za ndani kutoka mamlaka
ya mapato Tanzania(TRA) Bw.ELIJAH MWANDUMBYA alipokuwa katika uzinduzi wa
kampeni ya usajili wa walipakodi nchini kote iliyo fanyika Jijini DAR ES SALAAM
yenye lengo la kuongeza wigo na idadi ya walipakodi.
Amesema kuwa ni muhimu
kwa walipa kodi kuwa na namba hizo
kwani zinawasaidia kuepuka usumbufu
pindi wanapolipa kodi na hata kuhisaidia
mamlaka hiyo kukusanya mapato kwa urahisi bila usumbufu wowote.
Pia MWANDUMBYA amesisitiza kuwa usajili wa TIN namba kwa
walipa kodi ni bure na sio badala yake akatokea mtu akamdai mlipa kodi pesa
kwaajili ya kupata namba hizo kwani hatakau ameenda kinyume na utaratibu.
AIDHA ametoa wito kwa
walipa kodi kuwa hakuna wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili tin namba hivyo basi
usajili utafanyika katika ofisi za mamlaka hiyo na katika vituo maalum
ambavyo vitakuwa vimeteuliwa na kutangazwa kupitia vyombo vya habari
mabalimbali hapa nchini.
Post a Comment