Na.Martin Joseph
Asasi zisizo za
kiserikali hapa nchini zimetakiwa kutambua kuwa zinamchango mkubwa katika
utoaji wa takwimu hivyo nivyema wakendelea kutoa takwimu hizo kwakuzingatia
misingi,vigezo na sheria zilizo wekwa na ofisi ya taifa ya Takwimu ili kutoa
takwimu zenye uhakika na zisizokuwa na shaka yoyote.
Hayo yamesemwa na Mwanasheria kutoka katika ofisi ya taifa
ya Takwimu Bw.OSCAR MANGULA alipokuwa katika mkutano wa uzinduzi wa mapendekezo ya asasi za
kiraia na marekebisho ya sheria ya namba tisa ya takwimu ya mwaka 2015
uliyofanyika Jijini DAR ES SALAAM ambao umeandaliwa na jukwaa la maendeleo
endelevu(TSDP) kwakushirikaiana na taasisi ya inayojishugulisha na utohaji ushauri kwa asasi za kiraia barani
Afrika(APF).
Amesema ni vyema asasi hizo zikaizingatia sheria hiyo kwani
inawaelekeza kutoa takwimu ambazo zitakuwa rasmi na zenye kuwa na ukweli ndani yake hivyo asasi ambayo
itakuwa imekwenda kinyume na sheria hiyo itakuwa imekiuka misingi na sheria
zilizo wekwa na ofisi ya taifa ya takwimu na itachukiliwa hatua za kisheria kwakufuata adhabu ambazo
zimeorozeshwa katika sheria ya takwimu
namba tisa ya mwaka 2015 ambayo inaitaka
ofisi hiyo kutoa adhabu kwa mtu au chombo chochote kile ambacho kitakuwa
kimetoa takwimu za uhongo pasipo kufuata sheria.
Aidha nae mtafiti kutoka katika jukwaa la maendeleo
endelevu(TSDP) Bw.JOAKIM MANGILIMA ametoa usahuri kwa asasi zisizo kuwa za
kiserikali kutoa takwimu za kweli na ambazo zitaijenga jamii ili kuleta
maendeleo makubwa hapa nchini kupitia takwimu hizo.
Post a Comment