
Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia sheria bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini(HESLB) ambayo
inawataka kuwasilisha orodha ya majina ya waajiriwa wao ambao walikuwa ni
wanufaika wa bodi hiyo pindi walipokuwa vyuoni ili kuiwezesha bodi hiyo kajua
ni waajiriwa wangapi walikua wanufaika wa bodi hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu(HESLB) Bw.ABDULLAZAKI BADRU alipokuwa katika hafla
iliyofanyika Jijini DAR ES SALAAM ya kuwatambua baadhi ya waajiri wanao timiza
masharti ya bodi hiyo.
Amesema kuwa ni muhimu kila muajiri hapa nchini kuizingatia sheria hiyo kwani imekuwa ikiisadia bodi hiyo
kuongeza makusanyo kupitia waajiriwa
walikuwa ni wanufaika na hatimaye
kuwasaidi wanafunzi ambao bado wapo
vyuoni wanao hitaji mikopo kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.
Pia ametoa pongezi na
kuzikabidhi ngao baadhi ya kampuni na
taasisi ambazo zimekuwa zikitimiza mashariti na kuzingatia sheria za bodi ya
mikopo kwaiyo amezitaka kuendelea na
hali hiyo ili kusaidia makusanyo ya pesa
kupatikiana kwa urahisi bila matatizo yoyote kutoka waajiriwa wao.
Aidha nae Mkurugenzi Mtendaji wa urejeshaji wa mikopo kutoka
katika bodi hiyo Bw.PHIDELIS JOSEPH amesema kuwa wataendelea kuwatembelea
waajiri ili kubadilisha mawazo kwa lengo la kuongeza ufanisi na makusanyo na
hata kuwasikia na kubadilisha mawazo ili hatimaye nchi iwe na waajiri wengi
Zaidi wanaotimiza matwaka ya sheria ya bodi ya mikopo hapa nchini.
Post a Comment