0




 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhL6fyjns4EgR51NZIBx0SGNxLndKcHyc1aChfpWOunr7_RDU6fkoZM1bttFfuMFs4G7EeCiY69TQP0eG82Q5DRyCqFBRoKg1yDVKxcV11F_irp7YshsDox2Y1yRF8v-9PVmHdDVabUpIE7/s1600/1.JPG








Jeshi la polisi nchini limeombwa  kufanya kazi kwakushirikiana na wananchi pamoja na asasi za kiraia kwani kufanya hivyo watajiepusha kutumia nguvu kubwa na hata kuboresha dhana ya ulinzi shirikishi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalojishugulisha na kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwajengea uwezo wa kisheria na biashara wanawake walioko katika sekta zisizo kuwa rasmi hapa nchini(EFG) JANE MGIGITA alipokuwa akizungumza na waandishi wa  habari Jijini DAR ES SALAAM.

 Amesema kuwa ni vyema jeshi la polisi likatambua kuwa kufanya kazi zake kwa kwakuzingatia weledi,taaluma na sheria za nchi itawafanya  kuepukana na lawama pamoja na chuki kutoka kwa wananchi na hatimaye kuendelea kupata ushirikiano ambao utalifanya taifa kuendelea kuwa na Amani siku zote.

Aidha ameiomba Serikali itazame upya suala la upatikanaji wa Katiba mpya na mchakato wake uanze mwaka huu kwani ndiyo suluhisho la matatizo mbalimbali yanayotokea katika Jamii kwa sasa.


Post a Comment

 
Top