Na.Martin Joseph
Sekta binafsi na taasisi za fedha hapa nchini zimeombwa kuiunga mkono serikali katika mpango wake wa pili wa fedha jumuishi kwani kufanya hivyo itaisaidia serikali kuboresha maisha ya wananchi kupitia mpango huo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Bi.ASHATU
KIJAJI alipokuwa akimuwakilisha waziri wa wazira hiyo Mhe.PHILIP MPANGO katika
mkutano uliyofanyika Jijini DAR ES SALAAM wa ushirikishaji wa kifedha baina ya taasisi
ya kibenki inayo toa mikopo midogo midogo(FINCA MICRO FINANCE BANK) pamoja na taasisi ya kimataifa inayotoa
ushirikishaji wa kifedha na kuendeleza elimu kwa vijana barani Afrika(MASTER
CARD FOUNDATION).
Amesema kuwa mpango ulianziashwa na serikali kwa lengo la kufanikisha azima yake
ya kuwapatia wananchi maisha bora na kuwafanya
kuondokana na wiimbi la umaskini
na hatimaye waweze kupiga hatua
kimaendeleo wao na kwa taifa pia.
Aidha ametoa pongezi kwa kampuni za simu na mawasiliano hapa nchini kwani zimekuwa zikiwafikishia
wananchi huduma kwa urahisi na kwa haraka hivyo amezitaka sekta za fedha kuiga
mfano kwani watakua wamesaidia wananchi kwa kiasi kikubwa katika uapataji wa
fedha kwa kuboresha maisha yao.
Post a Comment