0



 https://pbs.twimg.com/media/DS1r6kNXUAA2xMO.jpg





 Na.Martin Joseph

 Wananchi na wadau wa sekta ya madini wametakiwa kuzingatia utaratibu wa kuwa na vibali vya usafirishaji wa madini kwenda nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Madini Mhe.DOTO BITEKO alipokuwa  akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jijini DRA ES SALAAM kuhusu mnada wa tatu wa mauzo ya Almasi za kampuni ya mgodi wa Williamson Diamond Limited uliyoafanyika nchini Ubeligiji .
Amesema kuwa kutokana na matatizo yanyojitokeza hapa nchini ya utohaji madini kiholela migodini pasipo kuwa na vibali ndio umepelekea kujengwa kwa ukuta kwenye mgodi wa mererani wenye urefu wa kilomita24.5 ambapo ujenzi huo utakamilika hivi punde.
Hivyo basi mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)kwa kushirikaiana na wataalam wa Wizara ya Madini imehamua kuanza zoezi la utohaji wa vitambulisho vya uraia kwa wananchi wa maeneo husika ili kusaidia kuondokana na tatizo hilo.
Aidha BITEKO ametoa wito kwa wananchi waliokua katika migodi mbalimabli kutoa ushirikaino kwa wizara hiyo pindi itakapo kuwa inaendesha zoazi hilo  kwakuwataja wale wote ambao watakua sio raia wa nchi hii ili wasiweze kupatiwa vitambulisho hivyo kwani lengo la vitambulisho hivyo ni kuzui  wizi wa madini na usafirishaji kiholela wa madini hayo na kulifanya Taifa kupata hasara kubwa na hata kudhalaulika.

Post a Comment

 
Top