0




 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmPOp8Fo9PkfWXQHX_fRCzbTCRrpCAGK5XSvlp7yLjKfclVFasM7gMkxPEvK-CDxllkfpAIMriplXNI9rkDABH4czigLZsNdUdYhyOpDk1y6PupQDwUkek7WF5LaHS8Ix4_pSEFoVrHYDW/s640/DSC09015.JPG
Jaji kiongozi wa mahakama kuu ya Tanzania Mhe.FERDINAND WAMBALI ameitaka kamati inayojishugulisha na utatuzi wa migogoro ya wafanyakazi(Utatu Endelevu) kufanya kazi pasipo kumtegemea mtu kwani kufanya ivyo itawasaidia wafanyakazikuodokana na changamoto zinazo wakabili.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kamati hiyo Jijini DAR  ES SALAAM amesema kumekuwa na migogoro mingi kwa wafanyakazi na hiiimekuwa ikipelekea wawekezaji wandani na hata wa nje kushindwa kushawishika kuwekeza katika makampuni na sekta mbalimbali.
Hivyo ni vyema kamati hiyo ikaendelea kufanya kazi kwa bidii pasipo kumtegemea mtu ili kuwasadia wafanyakazi kupata haki zao na hata kuwashawishi wawekezaji wa ndani  na wa nje  kujakuwekeza kwa wingi hapa nchini.
Aidha amelitaka shiriko la vyama vya  wafanyakazi(tucta)  kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi ikiwemo kutetea haki za wafanyakazi kwani wengi wao wamekuwa na migogoro inayowakabili ikiwemo kukosa kazi na manyanya kutoka kwa waajili wao hivyo nivyme wakaendelea kujadili nakukaa chini kuzitatua changamoto hizo.

Post a Comment

 
Top