
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo,alhaj Abdul Sharifu amefuta waraka uliotolewa wilayani hapo, ambao unakataza viongozi wa chama kutokuwa na fursa ya kuwahoji watendaji wa serikali.
Aliyasema hayo baada ya kufanyika sherehe za miaka 41 ya CCM katika kata za Mbwewe, Miono na Lugoba .
Alhaj Sharifu alisema waraka huo unasababisha baadhi ya watendaji kutowajibika ipasavyo kwa wananchi.
Alielezea waraka huo
unaonekana una maslahi ya watu binafsi ambao unakwenda kinyume na
maslahi ya wananchi hivyo hauna manufaa yoyote zaidi ya kuwakandamiza
wananchi.
“Naufuta maana
haiwezekani watendaji wa serikali waachwe wafanye wanavyotaka hata
wakiharibu tusiwahoji ,wakati chama kina wajibu wa watendaji wa serikali
,” alisema Sharifu.
Aidha Sharifu
alisema,baadhi ya mambo yamekuwa hayaendi kutokana na watendaji hao
kujisahau na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwani hakuna watu wa
kuwahoji.
“Kila siku Rais
anasisitiza chama ndiyo kimeunda serikali hivyo watendaji wake lazima
wasimamiwe na chama ,hatuwezi kuona mambo yanaharibika halafu tukae
kimya ikifika nyakati za uchaguzi tunaonekana hatujafanya lolote,Hili
halikubaliki,” alisema Sharifu.
Alisema ilani
inayotekelezwa ni ya CCM hivyo lazima viongozi wa CCM wasimamie
watendaji na hata ikiwezekana kuwaondoa wale ambao wanashindwa
kuwajibika kwenye nafasi zao.
Nae mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi, Abubakary Mlawa alisema wamejipanga vizuri
kuhakikisha miradi mbalimbali ya maenedeleo ya wananchi inakamilika kwa
muda uliopangwa.
Mlawa alisema kuwa
jumuiya zote za chama zimeungana kuhakikisha zinawatumikia wananchi kwa
kuhamasisha masuala ya maendeleo na kuibua miradi ya maendeleo ikiwa ni
pamoja na elimu, afya, maji, barabara, kilimo na mifugo.
Post a Comment