Mtandao
wa jinsia nchini(TGNP) Umeitaka serikali na wadau wengine wa maendeleo
kuwasaidia na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani
wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.
Akizungumza
Dar es Salaam leo Mratibu wa (TGNP) BI,JANE TESHA wakati wa warsha hiyo ya kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa
kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha
shughuli za biashara.
BI, JANE Amesema
ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika
uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.
Hata
hivyo Amesema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi
duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa
changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.
Post a Comment