Wito huo umetolewa na
kaimu mkurugenzi wa TaESA BONIFACE CHANDARUBA alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari Jijini DAR ES SALAAM kuhusu zoezi la utambuzi wa Watanzani wenye
taaluma na ujuzi katika sekta ya mafuta na gesi.
Amesema kumekuwa na tatizo la ajira kwa wananchi katika miradi mbalimbali inayoendelea hapa
nchini hivyo serikali kupitia mradi wa bomba la
kusafirisha mafuta ghafi
linalotoka nchini Ungada hadi Tanzania imehamua kutoa fursa nyingi za
ajira kwa wantanzani wenye taaaluma na ujuzi katika sekta hiyo kwa lengo la
kuwanufaisha wao binafsi na taifa kiujumla.
Pia ametoa wito kwa
wanafunzi wanao maliza vyuo vikuu kuacha tabia ya kusubili ajira kutoka
serikalini na badala yake wajiajili wenyewe kwani tatizo la ajira limekuwa
kubwa hapa nchini na duniani kote hivyo nivyema wakalitambulia hilo na
wakabadilika ili waweze kuondokana na tatizo hilo.
Aidha kwa upande mwingine nayo kampuni inayo jishugulisha na
uuzaji wa mbolea hapa nchini YARA
LIMITED imahamu kuiunga mkono serikali katika kufanikisha zoezi la uchumi wa viwanda linatimia
kwaku toa punguzo la bei kwa mbolea wanazozalisha kwa lengo la
kuwasaidia wakulima kuzalisha mazoa yakayokuwa bora na yenyetija
kwa maendeleo yao na hata ya Taifa.
Post a Comment